46 – Sulaymaan bin Harb ametuhadithia: Sa´iyd bin Zayd ametuhadithia, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Ka´b, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

صلوا عليَّ فإن صلاتكم عليَّ زكاة لكم، قال: وسلوا الله لي الوسيلة

”Niswalieni. Kwani hakika du´aa zenu kwangu ni utakaso kwenu.” Akasema: ”Na niombeeni kwa Allaah Njia (الوسيلة). Ima alituhadithia au tulimuuliza. Akasema: ”Njia ni ngazi ya juu zaidi Peponi. Hakuna atakayeipata isipokuwa mtu, na nataraji mimi ndiye mtu huyo.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi wake ni dhaifu kwa sababu ya Layth bin Abiy Sulaym, ambaye alikuwa akichanganya mambo. Hata Sa´iyd bin Zayd alikuwa na unyonge. Shariyk amesimulia kutoka kwake, lakini naye pia alikuwa mnyonge kama yeye. Ameipokea Ahmad (2/365). Lakini hata hivyo amefuatwa pia na Ibn Fudhwayl, ambaye ni mwaminifu. Ameipokea  Ibn Abiy Shaybah katika “al-Muswannaf” (2/217). Mu´tamar amewakhalifu na ameisimulia kutoka kwa Layth, kutoka kwa Ka´b, hali ya kukosekana Swahabah katika cheni ya wapokezi. Hivo ndivo amepokea mtunzi wa kitabu katika Hadiyth inayofuata. Kilicho karibu zaidi ni kuwa cheni ya wapokezi ni yenye kuungana. Hata hivyo ni yenye kuzungukia kupitia al-Layth ambaye hivi punde umekwishajua hali yake. Hata hivyo sehemu ya pili ya Hadiyth ni Swahiyh. Inatiliwa nguvu na Hadiyth ya Ibn ´Amr na itakuja huko mbele katika kitabu (50).

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 48-49
  • Imechapishwa: 18/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy