Wakadai kuwa Hadiyth inasema:
”Siku ya Qiyaamah Qur-aan itakuja katika umbile la kijana aliyepauka, itamjia mwenye nayo na kumwambia: ”Je, unanijua?” Atasema: ”Wewe ni nani?” Ndipo aseme: ”Wewe ni nani?” Aseme: ”Mimi ni Qur-aan ambaye nilikufanya kuhisi kiu katika michana yako na nikakufanya ukeshe nyusiku zako.” Ndipo imjie Allaah na kusema: ”Ee Mola! Alinisoma, akanielewa na kunitendea kazi.”
Wakadai kuwa Qur-aan imeumbwa kutokana na Hadiyth kama hizi. Tunawaambia kuwa sio Qur-aan ndio itakayokuja, isipokuwa thawabu za kile kisomo cha Qur-aan. Ni kama ile Hadiyth inayosema kwamba mwenye kusoma ”al-Ikhlaasw”, basi anapata thawabu kadhaa. Kwa sababu sisi tunasoma namna ambavo Qur-aan itasema:
”Ee Mola! Kwa sababu maneno ya Allaah hayaji, hayabadiliki kutoka hali moja kwenda nyingine. Ni thawabu za kisomo cha Qur-aan ndizo zitazokuja na kusema: ”Ee Mola![1]”
[1] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:
”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))
Ibn Taymiyyah amesema:
”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.” (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)
Ibn Kathiyr amesema:
”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))
Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:
”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))
- Muhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 166
- Imechapishwa: 01/05/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)