Wakadai kuwa Hadiyth inasema:

”Siku ya Qiyaamah Qur-aan itakuja katika umbile la kijana aliyepauka, itamjia mwenye nayo na kumwambia: ”Je, unanijua?” Atasema: ”Wewe ni nani?” Ndipo aseme: ”Wewe ni nani?” Aseme: ”Mimi ni Qur-aan ambaye nilikufanya kuhisi kiu katika michana yako na nikakufanya ukeshe nyusiku zako.” Ndipo imjie Allaah na kusema: ”Ee Mola! Alinisoma, akanielewa na kunitendea kazi.”

Wakadai kuwa Qur-aan imeumbwa kutokana na Hadiyth kama hizi. Tunawaambia kuwa sio Qur-aan ndio itakayokuja, isipokuwa thawabu za kile kisomo cha Qur-aan. Ni kama ile Hadiyth inayosema kwamba mwenye kusoma ”al-Ikhlaasw”, basi anapata thawabu kadhaa. Kwa sababu sisi tunasoma namna ambavo Qur-aan itasema:

”Ee Mola! Kwa sababu maneno ya Allaah hayaji, hayabadiliki kutoka hali moja kwenda nyingine.  Ni thawabu za kisomo cha Qur-aan ndizo zitazokuja na kusema: ”Ee Mola![1]

[1] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 166
  • Imechapishwa: 01/05/2024