44. Tofauti ya mwenye akili na asiyekuwa na akili

Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:

Hadiyth kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye akili ni yule ambaye anaibidisha nafsi yake na kufanyia kazi kwa yanayomgonja baada ya mauti na asiye muweza ni yule ambaye anafuata matamanio ya nafsi yake na huku akiwa na matumaini ya uongo kwa Allaah.”

Mwenye akili bi maana mwenye busara na mwenye maazimio ambaye anataka kuikoa nafsi yake.

Maneno yake:

“… ni yule ambaye anaibidisha nafsi yake.”

Bi maana anaihesabu nafsi yake duniani. Akaifanya hesabu nafsi yake, akasimama katika mpaka wake, akayatazama matendo yake; ikiwa ni matendo mema basi akayaendeleza, na ikiwa ni matendo maovu basi akaizuia nafsi yake.

Maneno yake:

“… na kufanyia kazi kwa yanayomgonja baada ya mauti.”

Ambayo ni kaburi, kufufuliwa, malipo, hesabu, Pepo na Moto. Kwa hiyo akafanya matendo mema ili asalimike kutokamana na adhabu ya kaburini, hali za siku ya Qiyaamah, adhabu ya Moto kwa njia ya kwamba akampwekesha Allaah, akamtakasia Yeye ´ibaadah, akatekeleza maamrisho ya Allaah, akasimama katika mipaka ya Allaah na akanyooka katika kumtii.

Maneno yake:

“… na asiye muweza ni yule ambaye anafuata matamanio ya nafsi yake… “

Akaichia nafsi yake kiholela ifanye itakacho na hajali. Ikafanya maovu na ikafanya mapungufu katika mambo ya wajibu:

“… na huku akiwa na matumaini ya uongo kwa Allaah.”

Akiwa na matumaini ya yeye kuwa kama muumini mwenye busara ambaye anaifanyia hesabu nafsi yake. Matumaini haya ni ya uongo na ni kujidanganya.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 74
  • Imechapishwa: 16/06/2022