44. Swawm – ngao ya wafanya ´ibaadah

253 – Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: Muhammad bin al-´Alaa’ bin Swaalih na wengine wamenihadithia, kutoka kwa al-Mubaarak bin Sa´iyd, kutoka kwa bwana mmoja, ambaye amesema:

”Tulifika kwa Abu Huswiyn akamwambia mke wake: ”Tupe ulichonacho.” Akamtumia sahani iliokuwa na mkate mwembamba, ambao tayari kuna mtu ameshakula sehemu yake, na kipande cha mfupa wa nyama. Akawaambia: ”Chukueni hiki. Naapa kwa Allaah hatuna kitu kingine.”

254 – Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: Ismaa´iyl bin Ziyaad amenihadithia:

”Bashshaar bin Bishr bin Surayd, ambaye alikuwa mfanya ´ibaadah, alitujia. Alikuwa hali isipokuwa matonge saba. Jioni moja nikamwendea ili kumsalimia, ambapo akanitolea tende nne na kusema: ”Kula hizo. Endapo tungelikuwa na zaidi basi badala yake tungelikupa nazo wewe.”

255 – Muhammad amesema: Hakiym bin Ja´far amenihadithia:

”Siku moja tulimwendea Misma´ bin ´Aaswim. Akanitolea bakuli dogo la zeituni lisilokuwa na mkate akasema: ”Kula hii. Naapa kwa Allaah sina mkate ambao unaweza kula pamoja nayo.”

256 – Muhammad amesema: Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Haarithiy amenihadithia:

”Bwana mmoja alikuja kwa al-Hasan bin Swaalih kumuuliza swali. Akaingia nyumbani kwake na hakuna alichopata isipokuwa chuchu ya unga. Akaitoa na kumpa nayo.”

257 – Muhammad amesema: Daawuud bin Muhabbar ametuhadithia: Matwar bin al-A´naq ametuhadithia, kutoka kwa Ziyaad an-Numayriy, ambaye amesema:

”Ilikuwa inasemwa kuwa starehe ya wafanya ´ibaadah ni kwa kiu kirefu na wa njaa, burudisho la macho yao ni urefu wa swalah ya usiku.”

258 – Muhammad amesema: Hakiym bin Ja´far amenihadithia: kutoka kwa Misma´, kutoka kwa al-Waliyd Abu Hishaam, kutoka kwa Budayl al-´Uqayliy, ambaye amesema:

”Swawm ni ngome ya fanya ´ibaadah.”

259 – Muhammad amesema: Hakiym bin Ja´far amenihadithia: Nimemsikia Mudhwar akisema:

”Naapa kwa Allaah! Hakuna moyo uliyohisi njaa ukakaribiwa na shaytwaan mpaka ataposhiba.”

260 – Muhammad bin Idriys amenihadithia: Muusa bin Ayyuub ametuhadithia: Dhwamrah ametuhadithia, kutoka kwa ash-Shaybaaniy, aliyesema:

”Wawakilishi wa wageni huko Yerusalemu walimtengenezea ´Umar bin al-Khattwaab chakula. Basi kila kunapokuja sahani ´Umar akawaa anaichukua na kuimimina juu ya nyingine. Bwana yule akamwambia: ”Sio hivo inavoliwa, ee Kiongozi wa waumini.” Akasema: ”Ole wako! Ni nani awezaye kuja na kukika hiyo kesho?”

261 – Muhammad amesema: Shu´ayb bin Mihraz ametuhadithia: ´Abdul-Waahid bin Zayd ametuhadithia:

”´Uqbah bin Saajj alikuwa kwenye karamu ya ndoa na akaletewa chakula. Kukawa kunatolewa sahani moja baada ya nyingine, ambapo akaanza kulia na kusema: ”Nilikutana na wa mwanzo wa ummah huu ambao walikuwa wakichelea jambo hili juu ya wale wataokuja baadaye.” Hivyo akala sahani moja peke yake.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 154-157
  • Imechapishwa: 02/08/2023