44. Dalili kuthibitisha kuwa nadhiri ni ´ibaadah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya nadhiri ni Kauli Yake (Ta´ala):

يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا

“Wale ambao wanatimiza nadhiri zao na wanaiogopa siku ambayo shari yake ni yenye kuenea.”[1]

Nadhiri ni kule kujilazimisha ´ibaadah ambayo mtu hakulazimishwa na Allaah. Nadhiri hiyo inaweza kuwa kwa kuachiwa na pia inaweza kufungamanishwa:

1 – Mfano wa nadhiri iliyoachiwa ni kama mtu kuweka nadhiri ya kuswali Rak´ah ishirini. Katika hali hiyo analazimika kutekeleza nadhiri yake. Mfano mwingine aweke nadhiri ya kutoa swadaqah pesa elfu kuwapa masikini. Katika hali hiyo pia ni lazima kwake kutekeleza nadhiri yake na kutoa swadaqah muda wa kuwa nadhiri hiyo ni ya utiifu. Ama ikiwa nadhiri ya maasi basi haijuzu kwake kutekeleza nadhiri yake.

2- Wakati mwingine nadhiri inakuwa ni yenye kufungamanishwa. Kwa mfano mtu aseme kuwa Allaah akimponya mgonjwa wake au mtoto wake akifaulu katika mtihani basi atatoa swadaqah kwa pesa elfu moja. Katika hali hiyo mtoto wake akifaulu au mgonjwa wake akaponya basi atalazimika kutoa swadaqah hiyo. Mfano mwingine aseme kuwa endapo mtoto wake atafaulu au anapona mgonjwa wake basi ataswali kwa ajili ya Allaah Rak´ah ishirini au atachinja kondoo na kumtoa swadaqah kuwapa mafukara. Katika hali hiyo ni lazima kwake kuto swadaqah.

Nadhiri hii ni ´ibaadah. Akitekelezewa asiyekuwa Allaah mtu anakuwa ameingia ndani ya shirki. Kwa mfano mtu aweke nadhiri ya kumchinjia aliyemo ndani ya kaburi au akaweka nadhiri ya kuswali kwa ajili ya mtu.

Msingi wa nadhiri ni jambo lenye kuchukiza. Kwa sababu mtu akiweka nadhiri anakuwa amejiwajibishia ´ibaadah ambayo Allaah hakumuwajibishia. Isitoshe pengine asiweze kuitekeleza. Kwa ajili hiyo amekataza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nadhiri na akasema:

“Usiweke nadhiri. Kwani hakika nadhiri haifai chochote kunako makadirio. Hakika mambo yalivyo ni kwamba hutoka kwa bakhili.”[2]

Hata hivyo anasifiwa pale atapoweka nadhiri na nadhiri hiyo ikawa ni ya utiifu kisha baadaye akaitekeleza. Kwa sababu Allaah (Ta´ala) amewasifu wema na akasema:

يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا

“Wale ambao wanatimiza nadhiri zao na wanaiogopa siku ambayo shari yake ni yenye kuenea.”[3]

[1] 76:07

[2] al-Bukhaariy (6693) na Muslim (1640).

[3] 76:07

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 69
  • Imechapishwa: 12/02/2023