43. Dalili kuthibitisha kuwa kuchinja ni ´ibaadah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya kuchinja ni Kauli Yake (Ta´ala):

قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ

“Sema: “Hakika swalah yangu, kichinjwa changu, uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah pekee, Mola wa walimwengu, hali ya kuwa hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza.”[1]

na katika Sunnah:

“Allaah amemlaani yule mwenye kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah.”[2]

MAELEZO

Kinacholengwa katika Aayah ni:

لِلَّـهِ

“… kwa ajili ya Allaah pekee.”

Vivo hivyo maneno Yake (Subhaanahu wa Ta´ala):

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ

”Basi swali kwa ajili ya Mola wako na [pia ukichinja] na chinja [kwa ajili Yake]!”[3]

Bi maana chinja.

Maneno yake mtunzi (Rahimahu Allaah):

“Allaah amemlaani yule mwenye kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah.”

Laana ni kufukuzwa na kuwekwa mbali na rehema za Allaah. Amelaaniwa kwa sababu ni mshirikina.

[1] 06:162-163

[2] Muslim (1978).

[3] 108:02

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 68
  • Imechapishwa: 12/02/2023