44. Atapokuwa Allaah siku ya Qiyaamah kwa mtazamo wa Jahmiyyah

Wakati Jahmiy huyu, alipoishiwa na hoja juu ya yale aliyoyadai kwa Allaah kwamba yuko pamoja na viumbe Wake, ndipo akalazimika kusema kuwa yuko katika kila kitu pasi na kugusa wala kujitenga. Tukawauliza ikiwa si mwenye kujitenga si ni mwenye kugusa kitu. Wakasema hapana. Tukawauliza ni vipi atakuwa katika kila kitu pasi na kuvigusa vitu hivyo wala kujitenga navyo. Hawakuweza kujibu. Wakasema halitakiwi kufanyiwa namna. Hatimaye wakawahadaa wajinga katika watu kwa maneno hayo ya hila.

Tukamuuliza kama siku ya Qiyaamah si atakuwa Peponi, Motoni, juu ya ´Arshi na hewani. Wakaitikia, ndio. Tukauliza ni wapi ambapo atakuwa Mola wetu. Akajibu kwamba atakuwa kila mahali kama ambavyo duniani alikuwa katika kila kitu. ´Aqiydah yenu ni kwamba ile sehemu ya Allaah ilioko juu ya ´Arshi basi iko juu ya ´Arshi, na ile sehemu ya Allaah ilioko Peponi basi itakuwa Peponi, ile sehemu ya Allaah ilioko Motoni basi itakuwa Motoni na ile sehemu ya Allaah ilioko hewani basi itakuwa hewani. Hivyo umebainika uwongo wao juu ya Allaah (´Azza wa Jall)[1].

[1] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 159-161
  • Imechapishwa: 30/04/2024