Ubainifu wa yale yanayosemwa na Allaah ndani ya Qur-aan:

إِنَّنِي مَعَكُمَا

“Hakika Mimi Niko pamoja nanyi.”[1]

Hili linaweza kuwa na maana nyingi, ikiwa ni pamoja na:

Allaah (´Azza  wa Jall) alisema kumwambia Muusa (´alayhis-Salaam):

إِنَّنِي مَعَكُمَا

“Hakika Mimi Niko pamoja nanyi.”[2]

Bi maana katika kuwatetea.

لاَ تَحْزَنْ إِنَّ اللّهَ مَعَنَا

“Usihuzunike – hakika Allaah yupamoja nasi!”[3]

Bi manaa katika kuwatetea.

كَم مِّن فِئَةٍ قَلِيلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً كَثِيرَةً بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ مَعَ الصَّابِرِينَ

“Makundi mangapi machache yameshinda makundi mengi kwa idhini ya Allaah? Na Allaah Yu pamoja na wenye kusubiri.”[4]

Bi maana katika kuwanusuru dhidi ya maadui wao.

فَلَا تَهِنُوا وَتَدْعُوا إِلَى السَّلْمِ وَأَنتُمُ الْأَعْلَوْنَ وَاللَّـهُ مَعَكُمْ

”Basi msinyong’onyee    mkataka suluhu, kwani nyinyi ndio mko juu. Na Allaah Yu pamoja nanyi.”[5]

Bi maana katika kuwanusuru dhidi ya maadui wao.

يَسْتَخْفُونَ مِنَ النَّاسِ وَلَا يَسْتَخْفُونَ مِنَ اللَّـهِ وَهُوَ مَعَهُمْ إِذْ يُبَيِّتُونَ مَا لَا يَرْضَىٰ مِنَ الْقَوْلِ

”Wanajificha watu wasiwaone na wala hawajifichi kwa Allaah ilihali yupamoja nao pale wanapokesha kupanga njama kwa maneno asiyoyaridhia.”[6]

Bi maana kwa utambuzi Wake juu yao.

فَلَمَّا تَرَاءَى الْجَمْعَانِ قَالَ أَصْحَابُ مُوسَىٰ إِنَّا لَمُدْرَكُونَ قَالَ كَلَّا ۖ إِنَّ مَعِيَ رَبِّي سَيَهْدِينِ

”Yalipoonana makundi mawili, wakasema watu wa Muusa: ”Hakika sisi bila shaka tutadirikiwa!” Akasema: ”Hapana! Hakika Mola wangu yupamoja nami ataniongoza.”[7]

Bi maana atanisaidia dhidi ya Fir´awn[8].

[1] 57:4

[2] 20:46

[3] 9:40

[4] 2:249

[5] 47:35

[6] 4:108

[7] 26:61-62

[8] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 158-159
  • Imechapishwa: 30/04/2024