43. Sera za Khawaarij wa leo ndio zilezile za wale wa kale

Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

72 – Kujiaminisha na kukata tamaa yote yanamtoa mtu nje ya Uislamu. Wale wanaoswali kuelekea Qiblah haki iko kati ya mambo hayo mawili.

73 – Mja hatoki nje ya imani isipokuwa kwa kukanusha kile alichokiingiza.

MAELEZO

Mshereheshaji Ibn Abiyl-´Izz (Rahimahu Allaah) amesema:

”Shaykh (Rahimahu Allaah) anaashiria kuwaraddi Khawaarij na Mu´tazilah, wenye kuona kuwa watenda madhambi makubwa wanatoka katika imani.”[1]

Mfano wa hawa ni wale watu ambao wanawakufurisha waislamu wote katika miji ya kiislamu, pasi na kubagua yoyote. Aidha wanawawajibishia wafuasi wao kujitenga na kuiacha miji hiyo. Kama walivofanya Khawaarij wa kale. Allaah awaongoze na awasamehe wale wachupaji wao ambao wao ndio walikuwa sababu ya upindaji huu wa khatari.

[1] Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 458

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 65-66
  • Imechapishwa: 02/10/2024