Kwa kumalizia ni kwamba ni wajibu kwa wanawake wote wajisitiri kwa jilbaab wanapotoka majumbani mwao. Hakuna tofauti katika hilo kati ya wanawake waungwana na wajakazi. Aidha inafaa kwao kuonyesha uso na mikono yake. Yalifanywa na wanawake wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yeye akawakubalia jambo hilo. Inaweza kuwa jambo lenye faida kunukuu mapokezi ya Salaf yanayotamka waziwazi kwamba jambo hilo lilikuwa lenye kufanyika hata baada ya kufariki kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Baadhi yake ni kama ifuatavyo:

1 – Qays bin Abiy Haatim amesema:

”Niliingia mimi na baba yangu kwa Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh). Alikuwa mweupe na mwembamba. Pembezoni naye alikuwepo Asmaa´ bint ´Umays ambaye alikuwa akimpepea. Alikuwa ni mwanamke mweupe aliyechanja mikono yake. Alimchanja katika kipindi kabla ya kuja Uislamu kama wanavofanya waberber. Akaonyeshwa farasi wawili na akaridhika nao. Mmoja nikampanda mimi na baba yangu akampanda mwingine.”[1]

[1] at-Twabariy katika “Tahdhiyb-ul-Aathaar”, Ibn Sa´d na at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” pasi na jumla isemayo:

”Alikuwa ni mwanamke mweupe aliyechanga mikono yake.”

Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 96
  • Imechapishwa: 24/09/2023