43. Mfungaji hahitajii kusukutua mdomo wakati wa kutawadha mchana wa Ramadhaan?

Swali 43: Je, ni sahihi kwamba mfungaji hahitajii kuzungusha maji mdomoni wakati wa kutawadha mchana wa Ramadhaan?

Jibu: Hilo si sahihi. Kuzungusha maji mdomoni wakati wa kutawadha ni faradhi miongoni mwa faradhi za wudhuu´. Ni mamoja mchana wa Ramadhaan au wakati mwingine kwa mfungaji na asiyekuwa mfungaji. Hilo ni kutokana na ueneaji wa maneno Yake (Ta´ala):

 فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ

“… basi osheni nyuso zenu… “[1]

Lakini hatakiwi kufanya kishindo katika kuzungusha maji mdomoni au kupalizia ilihali amefunga. Hayo ni kutokana na Hadiyth ya Laqiytw bin Swabirah ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia:

“Eneza vizuri wudhuu´, asua kati ya vidole na fanya kishindo katika kupalizia isipokuwa kama utakuwa umefunga.”

[1] 05:06

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 38
  • Imechapishwa: 30/04/2021