42. Mfungaji na dawa ya meno mchana wa Ramadhaan

Swali 42: Ni ipi hukumu kwa mfungaji kutumia dawa ya meno mchana wa Ramadhaan?

Jibu: Mfungaji kutumia dawa ya meno katika Ramadhaan na miezi mingine ni jambo halina ubaya ikiwa haikushuka tumboni mwake. Lakini bora ni kutoitumia. Kwa sababu inayo kemikali yenye nguvu inayoweza kupenyeza mpaka tumboni na mtu asihisi hilo. Kwa ajili hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia Laqiytw bin Swabirah (Radhiya Allaahu ´anh):

“Fanya kishindo katika kupalizia isipokuwa kama utakuwa umefunga.”[1]

Bora kwa mfungaji asitumie dawa ya meno. Jambo ni lenye wasaa. Endapo atachelewesha mpaka baada ya kukata swawm anakuwa ametimiza yale anayochelea yasije kuharibu funga yake.

[1] at-Tirmidhiy (788) na an-Nasaa´iy (87). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 38
  • Imechapishwa: 30/04/2021