44. Je, mfungaji anafungua kwa kudungwa sindani ya mishipa?

Swali 44: Je, mfungaji anafungua kwa kudungwa sindani ya mishipa?

Jibu: Mfungaji hafungui kwa kudungwa sindano kwenye mishipa au kwenginepo. Isipokuwa ikiwa sindano hizi zinasimama mahali pa chakula kwa njia ya kwamba mtu anaweza kujitosheleza kutokamana na chakula na kinywaji. Sindano za kawaida zisokuwa za lishe hazifunguzi kabisa. Ni mamoja sindano hizo zinadungwa kwenye mishipa au kwenginepo. Hilo ni kwa sababu sindano hizi sio kula wala kunywa na wala hazina maana ya kula na kunywa. Kujengea juu ya haya ni jambo linalokanushwa zikawa na hukumu ya kula na kunywa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 39
  • Imechapishwa: 30/04/2021