43. Kula viapo kwa makundi ya Kiislamu ni jambo la kizushi

2 – Viapo vya kizushi katika makundi ya Kiislamu. Viapo hivi ni  miongoni mwa vitu vilivyozuliwa katika mfumo wa kulingania. Wanazuoni wengi wamelikaripia na wakaandika juu yake vitabu kwa njia inayodhihirisha ubatilifu na upotofu wake. Miongoni mwao amesema Shaykh Bakr Abu Zayd (Rahimahu Allaah):

“Miongoni mwa mifumo inayochafua ulinganizi, kuchochea ghasia na kuufarikisha ummah makundimakundi, ni vile viapo vya utiifu vilivyozuliwa vinavyotoka kwa Suufiyyah na kuibuka katika makundi ya kiislamu. Namna hiyo ndivo yanakuwa matamanio; yanavutana. Kwa msemo mwingine ni kwamba katika Uislamu kuna kiapo kimoja tu cha utiifu, nacho anapewa yule kiongozi mkuu. Ni kile kiapo cha pamoja kinachotolewa na wale wanamme wenye maoni na ushawishi katika Ummah. Ni mamoja kiapo hicho kimetolewa kwa njia inayopendeza kwa Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama vile viapo walivyopewa makhaliyfah waongofu (Radhiya Allaahu ´anhum), au kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi. Kupitia kiapo hicho ndicho ambacho kiongozi na mtawala wa waislamu hufikia malengo ya utawala, ikiwa ni pamoja na nguvu, mamlaka na hatua. Matokeo yake akasimamisha hukumu ya Kiislamu kama vile kusimamisha adhabu za kidini, ugawaji wa mali, kuweka mamlaka, kupambana na adui, kusimamisha hajj, sikukuu, swalah za ijumaa na swalah za mikusanyiko na mengineyo katika yanayofupilizika na Shari´ah. Ummah siku zote ulipita katika jambo hilo. Viapo vingine vyote havikuwa vyenye kutambulika mbali na kile kiapo cha kiongozi mkuu.

Baadaye wakajitokeza warithi na mambo yaliyoosha ummah kama jinamizi la Bid´ah na mapote. Suufiyyah wakachangia kwa kiapo cha Furaha, Kiapo kilichobaguliwa, ahadi ya Mashaykh, mkataba wa mrengo na ahadi ya mrengo. Viapo vyote hivi ni vya kizushi na vimezuliwa. Havina dalili ndani ya Qur-aan, Sunnah wala matendo ya Maswahabah.

Muda ulipoenda jambo hili likahamia katika makundi ya kiislamu yaliyopo hii leo. Hali ikafikia kiasi cha kwamba wakati mwingine kunakuwa na makundi mengi ambayo yako na mikataba na ahadi katika mji mmoja. Kila kundi moja katika makundi hayo linalingania katika jambo lake ambapo ule mkataba wa Mtume “Ni lile litalofuata yale ninayofuata mimi hii leo na Maswahabah zangu” ukapotea. Namna hii ndivo mwili wa Ummah wa Kiislamu unavyokatwa, kuanzia viapo vya Suufiyyah juu ya harakati za kwenye pembepembe kwenda katika viapo vya vyama vya makubaliano na upinzani. Matokeo yake vijana wakawa ni wenye kudangana juu ya kwamba ni kipote kipi anatakiwa kujiunga nacho na ni mkuu wa chama gani anatakiwa kumpa kiapo cha usikivu.”[1]

[1] Hukm-ul-Intimaa’, uk. 161-163

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 53-55
  • Imechapishwa: 22/05/2023