244 – Muhammad bin Qudaamah al-Jawhariy amenihadithia: Sa´daan bin Jaamiy´ al-Jallaaba ametuhadithia, kutoka kwa Miskiyn Abu Faatwimah, kutoka kwa Swaalih al-Murriy, ambaye amesema:
”Nilisema kumwambia ´Atwaa´as-Saliymiy: ”Umekonda. Unasemaje tukufanyia supu ya maziwa?” Nikamtengenezea supu ya maziwa, ambapo akanywa kiasi. Kisha akafanya masiku kadhaa bila kunywa. Nikamwambia: ”Tumekupikia supu ya maziwa na imetupa tabu.” Akasema: ”Ee Abu Bishr! Mimi ninapokumbuka Moto basi sipati hamu.”
245 – Sa´iyd bin Sulaymaan ametuhadithia: Nimemsikia ´Abdullaah bin ´Abdil-´Aziyz al-´Umariy akisema:
”Mtu mmoja alimwambia ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Niusie.” Akasema: ”Tazama ni wapi unatoka mkate wako.”
246 – Muhammad bin al-Husayn amesema: Khalaf bin Tamiym ametuhadithia: Ibraahiym bin Ad-ham amesema:
”Muda wa kuwa chakula chako ni halali, hudhuriki kitu kwa kutoamka usiku kuswali na kufunga mchana.”
247 – Muhammad amesema: Hakiym bin Ja´far amenihadithia: Nimemsikia Abu ´Abdillaah al-Buraathiy amesema: ´Abdul-´Aziyz bin Abiy Rawwaad amesema:
”Tazameni mikate inayoingia matumboni mwenu; inatokea kwa wapi?”
248 – Muhammad amesema: as-Swalt bin Hakiym amenihadithia: Nimemsikia Abu Ja´far al-Mukhawwaliy akisema:
”Wakati mja anapohisi njaa, basi husafika mwili wake, hulainika moyo wake, machozi yake yakamtoka na viungo vyake vya mwili hufanya haraka kwenye utiifu, ambapo akaishi duniani akiwa mtukufu.” Kisha akasema: ”Maangamivu kwa yule ambaye amelitweza tumbo lake kwa sababu ya dini yake! Ole wake! Ole wake!”
- Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 149-151
- Imechapishwa: 01/08/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)