41. Chakula cha ´Iraaq ni zaidi ya supu ya maziwa

237 – Haaruun ametuhadithia: Sayyaar ametuhadithia: Ja´far ametuhadithia: Kahmas bin al-Hasan ametukhabarisha: Nimemsikia Bakr al-Muzaniy akisema:

”Kinakutosha katika dunia kile kinachokutosheleza, ijapo ni kiganja cha tende, glasi ya maji, kivuli cha hema. Kila ambavo utafungukiwa na kitu katika dunia, basi unazidi kuwa ni ufunguo juu yake.”

238 – Khalaf bin Saalim ametuhadithia: Abu Nu´aym ametuhadithia: Ismaa´iyl bin Ibraahiym bin Muhaajir ametuhadithia: Nimemsikia ´Abdul-Malik bin ´Umayr akisema: Mtu mmoja kutoka Thaqiyf amenihadithia:

”´Aliy aliniajiri ´Ukbarah, nikawa nimemwendea. Wakati nilipofika kwake, sikumpata mlinzi yeyote akimlinda. Nikamkuta ameketi chini akiwa na bakuli na kikombe cha maji. Akaniomba mfuko wa ngozi. Nikafikiria mwenyewe kuwa ameniamini sana kiasi cha kwamba anafikiriaa kunipa johari. Mfuko ule ulikuwa umefungwa. Akavunja ile kufuli. Mfuko ulikuwa na supu ya maziwa. Akaimwaga ndani ya chombo. Akanywa kutoka humo na kuninywesha na mimi. Sikuweza kusubiri ambapo nikasema: ”Ee kiongozi wa waumini! Unayafanya haya ´Iraaq? Chakula cha ´Iraaq ni zaidi ya hivo.” Akasema: ”Mimi hununua kile kiasi kinachonitosheleza. Sipendi kiharibike na kiwe kitu kingine. Sifungi mfuko kwa sababu ya uchoyo, isipokuwa ni kwa sababu ya kuuhifadhi. Mimi nachukia kuingiza tumboni mwangu isipokuwa tu kilicho halali.”

239 – Ishaaq bin Ibraahiym ametuhadithia: Hajjaaj bin Muhammad ametuhadithia, kutoka kwa Shariyk, kutoka kwa ´Aaswim bin Kulayb, kutoka kwa Muhammad bin Ka´b: Nimemsikia ´Aliy akisema:

”Nilikuwa pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati nafunga jiwe tumboni kutokana na njaa.”

240 – Abu ´Abdir-Rahmaan al-Qurashiy ametuhadithia: Abu Usaamah ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Abul-Jahhaaf, kutoka kwa bwana mmoja kutoka Khath´am, ambaye amesema:

”Niliingia kwa al-Hasan na al-Husayn na kuwaona wanakula mkate, siki na kunde.”

241 – Ishaaq bin Ibraahiym ametuhadithia: Jariyr ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa ´Amr bin Murrah, kutoka kwa Abu Swaalih, ambaye amesema:

”Niliingia kwa Umm Kulthum, ambapo akasema: ”Mleteeni Abu Swaalih chakula!” Wakaniletea mchuzi wenye nafaka ndani yake.”

242 – Ibraahiym bin al-Mundhir al-Hizaamiy ametuhadithia: ´Abdullaah bin Wahb ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Lahiy´ah, kutoka kwa ´Abdullaah bin Hubayrah, kutoka kwa ´Abdullaah bin Zurayr al-Ghaafiqiy, ambaye amesema:

”Tuliingia kwa ´Aliy bin Abiy Twaalib siku ya Adhwhaa. Akatuletea nyama kavu iliyokatwa.”

243 – Baba yangu amenihadithia: Sulaymaan bin Idriys al-Muqriy’ ametuhadithia:

”al-Hasan bin Hayy alitamani samaki. Wakati alipoletewa naye, akapiga kwa mkono wake tumboni mwa samaki kisha akaamrishwa aondoshwe. Hakumla chochote. Alipoulizwa sababu, akasema: ”Wakati nilipompiga tumbo lake, nimekumbuka kitu cha kwanza huoza kwa mtu ni tumbo lake. Ndio maana sikuweza kumuonja.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 146-149
  • Imechapishwa: 01/08/2023