42. Sunnah zinazoachwa na zisizoachwa safarini


Swali 42: Wametofautiana kuhusu ubora wa kuswali Sunnah za Rawaatib pamoja na kufupisha safarini. Wako wanaosema kuwa imependekeza kuiswali. Wengine wakasema kuwa haikupendekeza. Isitoshe wamefupisha zile swalah za faradhi. Unasemaje juu ya jambo hilo? Vivyo hivyo kuhusu ubora wa swalah zilizopendekezwa zilizoachiwa kama mfano wa swalah ya usiku[1].

Jibu: Sunnah kwa msafiri ni kuacha Raatibah ya Dhuhr, Maghrib na ´Ishaa pamoja na kuswali Sunnah ya Fajr kwa ajili ya kumwigiliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika jambo hilo. Vivyo hivyo imesuniwa kwake kuswali swalah ya usiku na kuswali Witr safarini. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya hivo. Hali kadhalika swalah nyenginezo zote zilizoachiwa na swalah zinazoswaliwa kutokana na sababu kama vile Sunnah ya Dhuhaa, Sunnah ya wudhuu´ na swalah ya kupatwa kwa jua. Vivyo hivyo imesuniwa kwake sijda ya kisomo na swalah ya mamkuzi ya msikiti akiingia msikitini kwa ajili ya kuswali au kwa lengo jengine. Basi atatakiwa kuswali swalah ya mamkuzi ya msikiti.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (11/391).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 58
  • Imechapishwa: 15/05/2022