41. Inafaa kukusanya Dhuhr na ´Aswr siku ya ijumaa


Swali 41: Je, inafaa kwa msafiri wakati anaposwali swalah ya ijumaa pamoja na wanyeji akaikusanya na ´Aswr[1]?

Jibu: Haijuzu kwake kufanya hivo. Kwa sababu swalah ya ijumaa haikusanywi na chochote. Bali ni lazima kwake kuswali ´Aswr ndani ya wakati wake. Lakini msafiri akiswali siku ya ijumaa Dhuhr na hakujaaliwa kuswali swalah ya ijumaa pamoja na wakazi, basi hapana vibaya kwake kuikusanya pamoja na ´Aswr. Kwa sababu msafiri hana swalah ya ijumaa. Jengine ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikusanya kati ya Dhuhr na ´Aswr katika hijjah ya kuaga siku ya ´Arafah kwa kutolewa adhaana moja na kukimiwa mara mbili na hakuswali ijumaa.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/300-301).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 57-58
  • Imechapishwa: 15/05/2022