43. Msafiri kukusanya swalah mwishoni mwa siku

Swali 43: Inafaa kwa muislamu akiwa ni msafiri safari ndefu akakusanya swalah mwishoni mwa siku[1]?

Jibu: Haya ni maovu makubwa. Hakuna mwanachuoni yeyote anayeonelea hivo. Mambo yalivo ni kwamba inafaa kwa msafiri kukusanya kati ya Dhuhr na ´Aswr peke yake katika wakati wa kimoja wapo kabla ya jua kuwa manjano, kati ya Maghrib na ´Ishaa katika wakati wa kimoja wapo kabla ya nusu usiku. Kuhusu Fajr haikusanywi na nyingine. Bali daima inaswaliwa ndani ya wakati wake safarini na katika hali ya ukazi kabla ya kuchomoza kwa jua.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/295-296).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 59
  • Imechapishwa: 15/05/2022