Kisha wanajitokeza walinganizi wa kimasoni ambao wanataka kuwarudisha watu katika hali za kinyama na usawa katika kila kitu. Wanapiga vita maadili mema na matendo mema. Lengo lao wasipambanue haki kutokamana na batili, kheri kutokaman na shari. Yote haya ni tofauti na yale waliyolingania kwayo Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Aidha ni tofauti ni yale yaliyojulishwa na Qur-aan tukufu ambayo ni miujiza. Vilevile ni tofauti na yale yaliyofahamishwa na akili timamu na maumbile yaliyosalimika ambayo Allaah amewaumba viumbe juu yake.

Hakika Allaah (Subhaanah) amewaumba watu kutambua maadili mema, matendo mema, uadilifu na haki. Sambamba na hayo amewaumba kwa maumbile ya kuchukia dhuluma na madhara. Allaah amewaumba waja katika maumbile ya kuweza kumpambanua baba kutokaman na mtoto, kaka kutokamana na dada, mke kutokamana na mume. Hata wanyama wanapambanua kati ya hiki na hiki.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamiyyat-ul-´Ilm https://binbaz.org.sa/discussions/33/اهمية-العلم-في-محاربة-الافكار-الهدامة
  • Imechapishwa: 15/05/2022