12. Radd kwa walinganizi wenye kuona kila kitu ni halali kufanya

Vivyo hivyo wale wanaoita katika propaganda za kuonelea kila kitu ni halali (لإباحيون) na kwamba hakuna neno kwa mtu – katika hali yoyote – kufanya anachotaka na kuhalalisha anachotaka katika mambo ya kipuuzi na mambo ya ovyo. Wote hawa ni wakanamungu na wapotofu. Allaah amebatilisha madhehebu haya. Amebainisha (Subhaanahu wa Ta´ala) ya kwamba ametumiliza Mitume na akateremsha Kitabu ili kubainisha haki yake juu ya waja Wake pamoja na yale mazuri aliyohalalisha, yale mabaya aliyoharamisha, yale ambayo (Subhaanahu wa Ta´ala) amewausia waja Wake katika kushikamana na yale waliyokuja nayo Mitume na kuyatupilia mbali yale yanayokwenda kinyume nayo. Ameweka wazi (Subhaanah) katika Vitabu Vyake vilivyoteremshwa kutoka mbinguni upambanuzi wa ya halali kutokamana na ya haramu, uongofu kutokamana na upotofu, mema kutokamana na maovu na kheri kutokaman na shari.

Wale wanaohalalisha kila kitu na wamasoni wameyapa mgongo yote hayo na kuyaweka nyuma ya migongo yao. Hakuna tabia njema yoyote waliyoshikamana nayo wala akili timamu waliyoshikamana nayo. Hawakuchukua yale yaliyoletwa na Mitume katika uongofu kutokamana na upotofu wala kupambanua kati ya haki na batili.

Yule ambaye atazingatia Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall) na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na pia akazingatia hali za ulimwengu, basi atatambua kuwa haki yote ni ile waliyokuja nayo Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) katika kubainisha yale aliyohalalisha Allaah, kubainisha yale aliyoharamisha (Subhaanah) na kwamba wametumilizwa ili wabainisha kati ya vile vizuri na vibaya, kati ya halali na ya haramu kwa yale aliyoyaweka Allaah katika Shari´ah. Lengo ni ili jamii ipite juu ya uongofu na ubainifu, kheri na mwongozo, maadili mema na sifa zinazosifiwa ambazo zinamlindia mtu akili na dini yake, mali na nafsi yake, kizazi chake, mke wake na wengineo. Ili asije akashambuliwa na wengine na hivyo jamii ikapata amani na hali na tabia ikanyooka barabara na watu wakapata amani. Matokeo yake kila mtu apate uhuru wake katika kuchukua na kutoa, kuuza na kununua na kutumia yale aliyomfanyia Allaah wepesi katika halali na kummilikisha vile alivyovichuma kwa njia zilizowekwa katika Shari´ah na kutumia vile vinavyomnufaisha na havimdhuru.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamiyyat-ul-´Ilm https://binbaz.org.sa/discussions/33/اهمية-العلم-في-محاربة-الافكار-الهدامة
  • Imechapishwa: 15/05/2022