Matapishi yakimshinda na akatapika bila kukusudia basi swawm yake ni sahihi na hakuna kinachomlazimu kufanya. al-Khaṭṭwaabiy amesema:

“Sijui kuwa kuna tofauti ya maoni kati ya wanazuoni kuhusu hili.”[1]

Ibn Qudaamah amesema:

“Haya ni maoni ya wanazuoni wote.”[2]

Maalik amepokea kutoka kwa Naafiy´, kutoka kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba alikuwa akisema:

“Mwenye kutapika kwa kukusudia ilihali amefunga, basi atalazimika kulipa.
Lakini mwenye kutapika bila kukusudia, basi hahitaji kulipa.”[3]

Wanazuoni wengine wanaona kuwa kutapika hakubatilishi swawm.. Haya ni maoni ya Ibn ‘Abbaas, Abu Hurayrah na Ibn Mas‘uud (Radhiya Allaahu ´anhum)[4]. Aidha ndivo anavosema ´Ikrimah. Dhahiri ni kwamba ndio chaguo la al-Bukhaariy pia, kwani amesimulia baadhi ya masimulizi yanayojulisha hilo. Ibn Hajar amesimulia upokezi kutoka kwa Maalik[5]. Dalili ya jambo hili ni kwamba hakuna chochote kilichosihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kuhusiana na jambo hili, japokuwa kutapika ni tatizo lililoenea na ummah unahitajika kujua hukumu ya jambo hilo.

Ibn-ul-Mundhir amepokea maafikiano ya kuharibika kwa swawm ya anayejitapisha[6] na Ibn Qudaamah[7] amenakili kutoka kwake, jambo ambalo linahitaji kuangaliwa vyema kwa sababu kumethibiti mitazamo tofauti, kama tulivyotangulia kusema – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

[1] Ma´aalim-us-Sunan (03/261).

[2] “al-Mughniy” (04/368).

[3] “al-Muwattwa´” (01/304) na cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh.

[4] Tazama “Muswannaf”” (01/170) ya ´Abd-ur-Razzaaq, ”al-Mughniy” (04/368) na ”Mawsu´atu Fiqh Ibn Mas´uud”, uk. 425.

[5] Fath-ul-Baariy (04/173-174).

[6] al-Ijmaa´ (35).

[7] al-Mughniy (04/368).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/55)
  • Imechapishwa: 25/02/2025