Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

nako ni kuomba wengine pamoja Naye. 

MAELEZO

Hii ndio maana ya shirki. Ni kule kuwaomba wengine pamoja Naye. Kwa msemo mwingine kufanya kitu katika ´ibaadah kumfanyia mwengine asiyekuwa Allaah katika Malaika, Mtume, mja mwema, jengo au kitu kingine katika viumbe. Yule mwenye kufanya kitu katika ´ibaadah akamfanyia mwengine asiyekuwa Allaah basi hilo ndio kubwa ambalo Allaah amekataza na pia ndio shirki. Kwa hiyo ujue maana ya Tawhiyd na maana ya shirki. Kwa sababu wapo watu ambao wanaifasiri Tawhiyd kinyume na tafsiri yake na wenye kuifasiri shirki kinyume na tafsiri yake.

Miongoni mwa watu wako wenye kusema kwamba shirki ni kule kushirikisha katika Haakimiyyah, jambo ambalo kwa masikitiko makubwa linaonekana hii leo. Kuhukumu kinyume na Shari´ah ya Allaah ni aina fulani ya shirki na inaitwa kuwa ni shirki ya utiifu. Hapana shaka kwamba kuwatii viumbe katika kuhalalisha yale aliyoharamisha Allaah au kuharamisha yale aliyohalalisha Allaah ni aina fulani ya shirki. Lakini kuna jambo ambalo ni kubwa zaidi kuliko hilo ambalo ni kumwabudu mwengine asiyekuwa Allaah (´Azza wa Jall) katika kuchinja, kuweka nadhiri, kutufu na kuomba msaada. Lililo la  wajibu ni kutahadharisha shirki yote na sio kuchukua sehemu yake na kuacha ambacho ni kikubwa na khatari zaidi kuliko. Shirki isifasiriwe kuwa ni shirki ya al-Haakimiyyah peke yake au shirki ya kisiasa na wanasema kuwa shirki ya makaburi ni shirki isiyokuwa na maana yoyote na kwamba ni nyepesi. Huku ni kuwa na ujasiri wa kipumbavu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Shirki ndio kubwa ambalo Allaah amekataza. Nayo ni kule kumuomba Allaah pamoja na wengine. Hii ndio shirki.

Miongoni mwao wako wengine wanaosema kuwa shirki ni kule kuipenda dunia na kupenda mali. Allaah ndiye ameifanya mali kupendwa mapenzi ya kimaumbile:

وَتُحِبُّونَ الْمَالَ حُبًّا جَمًّا

“Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi.”[1]

وَإِنَّهُ لِحُبِّ الْخَيْرِ

“… na hakika yeye ni mwingi mno wa kupenda [kukusanya] mali.”

Bi maana mali.

لَشَدِيدٌ

”… mwingi mno.”

قُلْ إِن كَانَ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَآؤُكُمْ وَإِخْوَانُكُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ وَعَشِيرَتُكُمْ وَأَمْوَالٌ اقْتَرَفْتُمُوهَا وَتِجَارَةٌ تَخْشَوْنَ كَسَادَهَا وَمَسَاكِنُ تَرْضَوْنَهَا أَحَبَّ إِلَيْكُم

“Sema: “Ikiwa baba zenu na watoto wenu na ndugu zenu na wake zenu na jamaa zenu na mali mliyoichuma na biashara mnayoikhofia kuharibika kwake na majumba mnayoridhika nayo –  [ikiwa vyote hivi] ni vipenzi zaidi kwenu.”[2]

Amesema kuwa ndio vinapendwa zaidi kwenu. Hakuwakataza kitendo chao cha kuvipenda. Lakini alichowakataza ni kule kutanguliza mapenzi yao juu ya mapenzi ya kumpenda Allaah. Kupenda mali sio shirki. Kwani haya ni mapenzi ya kimaumbile. Watu wanahitajia mali na wanaipenda. Kuipenda mali sio shirki. Kwa sababu ni katika kupenda manufaa ambayo watu wananufaika kwayo.

Lakini watu hawa wanaosema maneno haya ima ni wajinga hawakusoma Tawhiyd na shirki au ni wenye malengo fulani wanachotaka ni kuwazuia watu kutokamana na hakika hizi na kuwapeleka katika mambo wanayotaka – Allaah ndiye mjuzi zaidi wa malengo yao.

Muhimu ni kwamba mambo haya sio shirki. Shirki ni kule kumuomba asiyekuwa Allaah pamoja Naye au kufanya kitu katika aina za ´ibaadah kumfanyia mwengine asiyekuwa Allaah. Kwa mfano kuchinja, kuweka nadhiri, kuomba du´aa, kutaka uokozi, kutaka msaada, kuelekea, kuwa na khofu, kurejea na mengineyo. Hii ndio shirki ambayo ndio dhambi kubwa. Ni kule kuwaomba wengine pamoja Naye (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa sababu du´aa ndio aina kubwa ya ´ibaadah. Amesema (Subhaanahu wa Ta´ala):

لَهُ دَعْوَةُ الْحَقِّ ۖ وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَسْتَجِيبُونَ لَهُم بِشَيْءٍ

“Kwake ndiko kunaelekezwa maombi yote ya haki. Na wale wanaoomba pasi Naye hawawaitikii kwa chochote.”[3]

فَادْعُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ

“Basi mwombeni Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini, japokuwa wanachukiwa makafiri.”[4]

Kumuomba asiyekuwa Allaah ndio shirki ambayo ameiharamisha Allaah na Mtume Wake. Kuhusu vijisehemu hivi wanavyovifanya kuwa ni shirki mambo sivyo. Lakini kunasemwa kwamba baadhi yavyo ni sehemu ya ushirikina. Sambamba na hilo kuna ambayo ni khatari na muhimu zaidi kuliko hayo. Kwa sababu shirki inatofautiana; baadhi yake ni khatari zaidi kuliko nyingine.

[1] 89:20

[2] 09:24

[3] 13:14

[4] 40:14

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 88-90
  • Imechapishwa: 14/12/2020