40. Kulinganisha upande wa kulia mwa safu na kushotoni mwake

Swali 40: Je, safu inaanza kuliani au nyuma ya imamu? Je, imesuniwa kulinganisha kati ya upande wa kulia na upande wa kushoto wa safu kwa njia ya mtu kufikia kuwaambia waswaliji wasawazishe safu? Hayo yanafanywa na maimamu wengi.

Jibu: Safu inaanza katikati pale anapoanzia imamu. Upande wa kulia wa kila safu ni bora kuliko kushotoni mwake. Kilicho cha lazima isianzishwe safu mpaka ikamilishwe ya kabla yake. Hapana neno watu wakawa wengi upande wa kuliani mwa safu. Hapana haja ya kusawazisha. Bali kuamrisha jambo hilo kunaenda kinyume na Sunnah. Hata hivyo kusianzishwe safu ya pili mpaka ikamilishwe ya kwanza, wala ya tatu mpaka ikamilishwe ya pili na kadhalika safu zilizosalia. Kumethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maamrisho ya kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 47-48
  • Imechapishwa: 29/08/2022