40. Kisomo cha Qur-aan katika swalah ya ijumaa

8- Swalah ya ijumaa

Wakati fulani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisoma Suurah “al-Jumu´ah” katika Rak´ah ya kwanza na “al-Munaafiquun” katika Rak´ah ya pili. Wakati mwingine akisoma badala yake “al-Ghaashiyah”[1].

Wakati mwingine ilikuwa ikitokea akisoma (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) “al-A´laa” katika ya kwanza na “al-Ghaashiyah” katika ya pili[2].

[1] Muslim na Abuu Daawuud. Imetajwa katika ”al-Irwaa’” (345).

[2] Muslim na Abuu Daawuud. Imetajwa katika ”al-Irwaa’” (345).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 107
  • Imechapishwa: 15/02/2017