7- Witr

Katika Rak´ah ya kwanza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anasoma “al-A´laa”, “al-Kaafiruun” katika Rak´ah ya pili na “al-Ikhlaasw” katika Rak´ah ya tatu[1]. Mara nyingine alikuwa akiongezea Suurah “al-Falaq” na “an-Naas”[2].

Mara nyingine ilikuwa ikitokea (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisoma Aayah mia moja kutoka katika Suurah “an-Nisaa´” pindi anaposwali Witr[3].

Kuhusiana na Rak´ah mbili baada ya Witr[4], akisoma (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndani yazo Suurah “az-Zalzalah” na “al-Kaafiruun”[5].

[1] an-Nasaa’iy na al-Haakim aliyeisahihisha.

[2] at-Tirmidhiy, Abuul-´Abbaas al-Aswamm (2/117) na al-Haakim ambaye kaisahihisha na adh-Dhahabiy kaafikiana naye.

[3] an-Nasaa’iy na Ahmad kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh.

[4] Rak´ah mbili hizi zimethibiti katika ”as-Swahiyh” Muslim na wengineo. Hata hivyo zinakwenda kinyume na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ifanyeni swalah yenu ya mwisho usiku iwe ni Witr.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim. Wanachuoni wamejaribu kuzioanisha kwa njia mbalimbali. Hata hivyo sijakinaika na mtazamo hata mmoja na kwa ajili hiyo lililo salama zaidi ni kufuata amri na kutoziswali na Allaah ndiye anajua zaidi.

Baadaye nikaja kupata Hadiyth Swahiyh inayoamrisha kuswali Rak´ah mbili baada ya Witr na hivyo amri ikaafikiana na kitendo chake na kwamba ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa watu wote kuswali Rak´ah mbili hizi. Ina maana ya kwamba amri ya kwanza inaashiria mapendekezo na kwa ajili hiyo hakuna mgongano. Nimeitaja katika “as-Swahiyhah” (1993) na himdi zote anastahiki Allaah.

[5] Ahmad, Ibn Naswr, at-Twahaawiy (1/202), Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan kwa mlolongo wa wapokezi mzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 106-107
  • Imechapishwa: 15/02/2017