Maneno yake:

“Hakuna yeyote awezaye kuiepuka Qadar.”

Hakuna njia ya kukwepa Qadar iliyopangwa. Lakini nyinyi mlichoamrishwa ni kufanya sababu. Ama uumbaji wa natija ni jambo liko mikononi mwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Unaweza kufanya na usipate kitu kwa sababu Allaah hakukukadiria natija. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pupia yale yenye kukunufaisha na mtake msaada Allaah na wala usishindwe. Ukifikwa na jambo, basi usisemi “Laiti ningefanya hivi na hivi ingelikuwa hivi na hivi.” Lakini badala yake sema:

قدر الله وما شاء فعل

“Qadar ya Allaah; akitakacho huwa.”[1]

Wewe fanya sababu tu na masuala ya kufikia malengo ni jambo liko kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Usipofikia malengo basi usiilaumu nafsi yako. Kwa sababu umefanya uwezacho na unaamini mipango na makadirio ya Allaah. Isemeze nafsi yako kwamba pengine Allaah amekuchagulia kilicho na kheri nawe na kwamba pengne ungefikia malengo yako ingekuwa madhara kwako. Hivyo Allaah amenikinga kwa ajili ya manufaa yangu. Kwa hiyo usichukie jambo hilo.

[1] Muslim (2664) kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 61
  • Imechapishwa: 23/03/2021