Swali 38: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alishukia wapi Madiyanah?
Jibu: Alipofika Madiynah na kila mmoja Madiynah katika Wanusuraji akimkaribisha ashukie kwake, alisema:
”Mwache. Anaamrishwa.”
Bi maana ngamia wake.
Hatimaye akaegesha maeneo ambapo baadaye ulijengwa msikiti wake. Abu Ayyuub Khaalid bin Zayd akampokea mzigo wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikaa kwake mpaka alipojenga msikiti wake na makazi yake – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
- Muhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 106
- Imechapishwa: 04/10/2023