Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

63 – Hatuingii katika maneno ya kipuuzi kuhusu Allaah na wala hatuvutani kuhusu dini ya Allaah.

64 – Hatubishani juu ya Qur-aan. Tunashuhudia kuwa ni maneno ya Mola wa walimwengu.

65 – Ameteremka nayo roho mwaminifu akamfunza nayo bwana wa Mitume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

66 – Nayo ni maneno ya Allaah (Ta´ala) na hayalingani chochote na maneno ya viumbe.

67 – Hatuoni kuwa imeumbwa na wala hatuendi kinyume na mkusanyiko wa waislamu.

MAELEZO

Hakika miongoni mwa mtihani mkubwa uliowapata baadhi ya mapote ya Kiislamu kwa sababu ya elimu ya falsafa, imewapindisha kutokana na kuamini ya kwamba Qur-aan Tukufu ni maneno ya kikweli ya Mola wa walimwengu na si mafumbo. Kuhusu Mu´tazilah, wanaosema kuwa Qur-aan imeumbwa, jambo lao liko wazi la limefichuliwa. Hata hivyo kuna kundi ambalo linajinasibisha na Sunnah na ambalo linawaraddi Mu´tazilah kutokana na ´Aqiydah hiyo na nyenginezo ambalo limepinda kutokana na Uislamu – nao si wengine ni Ashaa´irah na Maaturiydiyyah. Uhakika wa mambo ni kwamba wanaafikiana na Mu´tazilah wanaosema kuwa  Qur-aan imeumbwa na kwamba si maneno ya Mola wa walimwengu. Isipokuwa tu wao hawayatamki hayo waziwazi. Wanajificha nyuma ya ´Aqiydah yao ya kwamba maneno ya kiungu ni maneno ya kindani na ya kale yasiyoweza kusikika na yeyote, si kwa Malaika wala Mitume. Aidha wanadai kuwa Allaah (Ta´ala) hazungumzi pale anapotaka na kwamba anazungumza tangu hapo kale.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 56-57
  • Imechapishwa: 30/09/2024