Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
59 – Amewafanya viumbe Wake wasiweze kuyazunguka.
60 – Tunaamini kuwa Allaah amemfanya Ibraahiym kuwa kipenzi wa hali ya juu na amemzungumzisha Muusa maneno ya kweli. Tunayaamini hayo, kuyathibitisha na kujisalimisha nayo.
61 – Tunawaamini Malaika, Mitume na Vitabu walivyoteremshiwa Mitume. Tunashuhudia ya kwamba vilikuwa vya haki ilio wazi.
62 – Tunawaita wale wanaoswali kuelekea Qiblah chetu kuwa ni ”waislamu” na ”waumini”, muda wa kuwa wanatambua yale yaliyokuja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanasadikisha yale yote aliyoyasema na kuyaeleza.
MAELEZO
Mshereheshaji Ibn Abiy-´Izz (Rahimahu Allaah) amesema:
”Shaykh (Rahimahu Allaah) anaashiria kuwa Uislamu na imani ni kitu kimoja, na kwamba muislamu hatoki nje ya Uislamu kwa kutenda dhambi, muda wa kuwa haihalalishi. Makusudio ya ”wale wanaoswali kuelekea Qiblah chetu” wanakusudiwa wale wote wanaojinasibisha na Uislamu na wanaswali kuelekea Ka´bah, pasi na kujali ni katika wazushi au watenda madhambi, muda wa kuwa hawajakadhibisha chochote katika yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[1]
[1] Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 426-427
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 55
- Imechapishwa: 30/09/2024
Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
59 – Amewafanya viumbe Wake wasiweze kuyazunguka.
60 – Tunaamini kuwa Allaah amemfanya Ibraahiym kuwa kipenzi wa hali ya juu na amemzungumzisha Muusa maneno ya kweli. Tunayaamini hayo, kuyathibitisha na kujisalimisha nayo.
61 – Tunawaamini Malaika, Mitume na Vitabu walivyoteremshiwa Mitume. Tunashuhudia ya kwamba vilikuwa vya haki ilio wazi.
62 – Tunawaita wale wanaoswali kuelekea Qiblah chetu kuwa ni ”waislamu” na ”waumini”, muda wa kuwa wanatambua yale yaliyokuja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanasadikisha yale yote aliyoyasema na kuyaeleza.
MAELEZO
Mshereheshaji Ibn Abiy-´Izz (Rahimahu Allaah) amesema:
”Shaykh (Rahimahu Allaah) anaashiria kuwa Uislamu na imani ni kitu kimoja, na kwamba muislamu hatoki nje ya Uislamu kwa kutenda dhambi, muda wa kuwa haihalalishi. Makusudio ya ”wale wanaoswali kuelekea Qiblah chetu” wanakusudiwa wale wote wanaojinasibisha na Uislamu na wanaswali kuelekea Ka´bah, pasi na kujali ni katika wazushi au watenda madhambi, muda wa kuwa hawajakadhibisha chochote katika yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[1]
[1] Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 426-427
Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 55
Imechapishwa: 30/09/2024
https://firqatunnajia.com/37-wale-wanaoswali-kuelekea-qiblah-chetu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)