Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
58 – Amekizunguka kila kitu na Yeye yuko juu yake.
MAELEZO
Matoleo ya sentesi isemayo ”na Yeye yuko juu yake” yametofautiana. Toleo la Ibn Abiyl-´Izz imekuja kama unavyoona hapo juu. Katika baadhi ya nakala na katika chapa ya Shaykh Ibn Maaniy´ imekuja ” Yeye yuko juu yake.” Katika nakala zingine imepotoka kabisa jumla ”na yale yaliyoko juu yake”. Hizi mbili za mwisho zilizotajwa ni dhaifu inapokuja katika masimulizi na maana. Ni dhaifu inapokuja katika masimulizi kwa sababu zinapingana na nakala zilizo nyingi, na ni dhaifu inapokuja katika maana kwa sababu mshereheshaji amesema:
”Nuskha ya kwanza ndio sahihi.”[1]
Maana ya nuskha ya kwanza ni kwamba Yeye (Ta´ala) amekizunguka kila kitu na Yuko juu ya kila kitu. Maana ya nuskha ya pili ni kwamba amekizunguka kila kitu kilicho juu ya ´Arshi. Jambo hili ima iwe ni kosa la uchapishaji kwa kutokukusudia, na baadaye wakayanakili baadhi ya watu, au iwe baadhi ya wakengeushaji na wapotevu wamefanya hivo kwa makusudi kwa ajili ya kupinga ujuu wa Allaah. Vinginevyo dalili zimefahamisha kuwa ´Arshi iko juu ya viumbe wote na kwamba hakuna kiumbe chochote kilicho juu zaidi kuliko ´Arshi. Jumla isemayo ”Amekizunguka kila kitu kilicho juu ya ´Arshi” isingelikuwa na maana yoyote, kwa sababu hakuna kiumbe chochote kilichoko juu ya ´Arshi kinachozungukwa. Kwa hivyo toleo linalosema ”na Yeye yuko juu yake” ndio sahihi zaidi. Hivyo maana yake inakuwa kwamba Allaah amekizunguka kila kitu na kwamba Yeye yuko juu ya kila kitu.
[1] Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 281
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 53-54
- Imechapishwa: 30/09/2024
Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
58 – Amekizunguka kila kitu na Yeye yuko juu yake.
MAELEZO
Matoleo ya sentesi isemayo ”na Yeye yuko juu yake” yametofautiana. Toleo la Ibn Abiyl-´Izz imekuja kama unavyoona hapo juu. Katika baadhi ya nakala na katika chapa ya Shaykh Ibn Maaniy´ imekuja ” Yeye yuko juu yake.” Katika nakala zingine imepotoka kabisa jumla ”na yale yaliyoko juu yake”. Hizi mbili za mwisho zilizotajwa ni dhaifu inapokuja katika masimulizi na maana. Ni dhaifu inapokuja katika masimulizi kwa sababu zinapingana na nakala zilizo nyingi, na ni dhaifu inapokuja katika maana kwa sababu mshereheshaji amesema:
”Nuskha ya kwanza ndio sahihi.”[1]
Maana ya nuskha ya kwanza ni kwamba Yeye (Ta´ala) amekizunguka kila kitu na Yuko juu ya kila kitu. Maana ya nuskha ya pili ni kwamba amekizunguka kila kitu kilicho juu ya ´Arshi. Jambo hili ima iwe ni kosa la uchapishaji kwa kutokukusudia, na baadaye wakayanakili baadhi ya watu, au iwe baadhi ya wakengeushaji na wapotevu wamefanya hivo kwa makusudi kwa ajili ya kupinga ujuu wa Allaah. Vinginevyo dalili zimefahamisha kuwa ´Arshi iko juu ya viumbe wote na kwamba hakuna kiumbe chochote kilicho juu zaidi kuliko ´Arshi. Jumla isemayo ”Amekizunguka kila kitu kilicho juu ya ´Arshi” isingelikuwa na maana yoyote, kwa sababu hakuna kiumbe chochote kilichoko juu ya ´Arshi kinachozungukwa. Kwa hivyo toleo linalosema ”na Yeye yuko juu yake” ndio sahihi zaidi. Hivyo maana yake inakuwa kwamba Allaah amekizunguka kila kitu na kwamba Yeye yuko juu ya kila kitu.
[1] Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 281
Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 53-54
Imechapishwa: 30/09/2024
https://firqatunnajia.com/36-kosa-la-uchapishaji-au-maharibifu-ya-kukusudia-katika-at-twahaawiyyah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)