37. Aina ya saba ya majina yaliyochukizwa

7- Imechukizwa kuitwa kwa jina la mnyama anayejulikana kwa sifa twevu. Mfano wa majina haya ni kama Hanash (nyoka), Himaar (punda), Qunfudh, Qunayfidh (mnyama aina kama ya panya aliye na manyoa mengi), Qirdaan (ngedere wawili), Kalb (mbwa) na Kulayb (kijibwa kidogo). Pindi waarabu wa kale walipowapa watoto wao majina haya ilikuwa ni kwa sababu ya zile sifa nzuri zinazopatikana katika wanyama hawa. Kwa mfano mbwa iko na umakini na bidii, punda iko na uvumilivu na subira. Kwa ajili hiyo ikawa matusi ya watu kwa waarabu yakawa yamepotea, yamesemwa na Ibn Durayd, Ibn Faariys na wengineo.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 27
  • Imechapishwa: 18/03/2017