38. Aina ya nane ya majina yaliyochukizwa

8- Aina ya nane ya majina yaliyochukizwa ni kila jina lililo na neno “ad-Diyn” (dini) au “al-Islaam” (uislamu) kama mfano wa Nuur-ud-Diyn (nuru ya dini), Dhiyaa´-ud-Diyn (mwanga wa dini), Sayf-ul-Islaam (upanga wa Uislamu), Nuur-ul-Islaam (nuru ya Uislamu) na kadhalika. Hilo ni kwa sababu neno “ad-Diyn” na “al-Islaam” ni kubwa na majina yaliyo na tamko hili ni madai ya kina yenye kunuka uongo. Kwa ajili hiyo baadhi ya wanachuoni wameharamisha majina kama hayo ilihali wengi wao wanaonelea kuwa ni yenye kuchukizwa. Majina kama hayo yanatoa maana isiyokuwa sahihi ambayo haijuzu kuitamka. Mwanzoni yalikuwa yakitumiwa kama jina la utani, halafu baadae yakaja kuwa kama majina ya kawaida.

Isitoshe majina kama haya yanaweza kuwa yamekatazwa kwa njia mbili. Mfano wa majina hayo ni Shihaab-ud-Diyn (moto wa dini). Indonesia wamefikia kiasi cha kwamba watu wanaitwa Dhahab-ud-Diyn (dhahabu ya dini) na Maas-ud-Diyn (almasi ya dini).

an-Nawawiy alikuwa akichukia jina lake la utani Muhyiy-ud-Diyn (muhuishaji wa dini) na Shaykh-ul-Islaam (Rahimahumaa Allaah) alikuwa akichukia jina lake la utani Taqiyy-ud-Diyn (mchaji Allaah wa dini) na akisema:

“Lakini familia yangu ndio ilinipa jina hilo na likawa maarufu.”

Mtu wa kwanza aliyepata laqabu kama hiyo katika Uislamu alikuwa ni Ibn Buuyah aliyekuwa akiitwa “Rukn-ud-Diyn” (nguzo ya dini). Ilikuwa katika karne ya nne.

Mfano mwingine wa majina ya kupindukia ni “Zayn-ul-´Aabidiyn” (uzuri wa wenye kuabudu), walilokuwa wakilifupisha kwa “Zaynal”, na “Qasaam ´Aliy” (uzuri wa ´Aliy), walilokuwa wakilifupisha kwa “Qasamliy”. Na khaswa wakazi wa Baghdad wanafupisha majina “Sa´d-ud-Diyn”, “´Izz-ud-Diyn” na “´Alaa-ud-Diyn” kwenda Sa´diy, ´Izziy na ´Alaaiy.

Raafidhwah wanataja kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpa ´Aliy bin al-Husayn bin ´Aliy bin Abiy Twaalib (Rahimahu Allaah) laqabu “Sayyid-ul-´Aabidiyn” (kiongozi wa wenye kuabudu). Hata hivyo halina asli, kama alivyosema Ibn Taymiyyah katika “Minhaj-us-Sunnah” na Ibn-ul-Jawziy katika “al-Mawdhuu´aat”. ´Aliy bin al-Husayn alikuwa ni katika waliokuja baada ya Maswahabah – ni vipi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliweza kumpa laqabu? Allaah awaue Raafidhwah! Ni waongo wakubwa waliyoje na ni wahamnazo waliyoje!

Katika majina mabaya kabisa niliyosikia ni majina yao “Jalbullaah” ikiwa na maana ya “Kalbullaah” (mbwa wa Allaah) kwa lahja ya kiiraki. Baadhi ya Raafidhwah wanaitwa “Jalb ´Aliy”, bi maana “Kalb ´Aliy” (mbwa wa ´Aliy). Malengo ya jina hilo ni yule mpewaji jina awe ni mwaminifu kama jinsi mbwa ilivyo aminifu kwa bwana wake.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 27-28
  • Imechapishwa: 18/03/2017