Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Maana ya “waniabudu” ni wanipwekeshe.

MAELEZO

Maana ya ´waniabudu` ni wanipwekeshe – Bi maana wanipwekeshe kwa ´ibaadah. ´Ibaadah na Tawhiyd maana zake ni moja. Tawhiyd inafasiriwa kwa ´ibaadah na ´ibaadah inafasiriwa kwa Tawhiyd. Maana zake ni moja. Hapa kuna Radd kwa wale waliofasiri Tawhiyd kwamba maana yake ni kukubali kwamba Allaah ndiye muumbaji, mruzukaji, muhuishaji, mfishaji na mwendesha mambo. Hii sio Tawhiyd ambayo viumbe wameumbwa kwa ajili yake. Viumbe wameumbwa kwa ajili ya Tawhiyd-ul-´Ibaadah ambayo pia ni Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah. Kuhusu ambaye anakubali Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah peke yake sio mpwekeshaji na sio katika watu wa Peponi. Bali ni katika watu wa Motoni. Kwa sababu hakuleta Tawhiyd ambayo ndio ambayo viumbe wameumbwa kwa ajili yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 79
  • Imechapishwa: 09/12/2020