Khofu na matarajio hutembea kwa muumini kama mbawa za ndege. Ndege inakuwa na mbawa mbili. Mbawa zote mbili zikiwa sawa, basi ndege huwa sawa. Mbawa moja kati ya hizo mbili ikiingiwa na kasoro, basi zote mbili huingiwa na kasoro na anakuwa katika khatari ya kifo. Vivyo hivyo ndivo anakuwa muumini moyo wake unatembea kati ya khotu na matarajio. Anayetembea kwa khofu pasi na matarajio, anaangamia. Muumini anapokuwa na khofu peke yake bila ya kutaraji, basi khofu yake inampelekea kumdhania Allaah vibaya na kukata tamaa na faraja ya Allaah. Vivyo hivyo kuwa na matarajio peke yake. Upande wa matarajio ukiwa na nguvu zaidi basi anayadogesha maasi na anakuwa si mwenye kujali wala kuogopa. Muumini anakuwa mwenye kuogopa. Hata hivyo kuogopa kwake hakumpelekei kukata tamaa na kuvunjika moyo. Kwa sababu anataraji na kutaraji. Hata hivyo matarajio yake hayampelekei kuyadogesha maasi.

Ni lazima moyo wa muumini uunganishe khofu na matarajio ili matarajio yake yasimpelekei kujiaminisha na vitimbi vya Allaah au khofu yake ikampelekea kukata tamaa na rehema za Allaah. Ndio maana sifa ya rehema ikatajwa sambamba na sifa ya adhabu katika maeneo mengi ndani ya Qur-aan ili kumfanye muumini kuwa na nguvu katika khofu na kutaraji na kuwa kati na kati baina ya msamaha na makemeo Yake. Amesema (Subhaanahu wa Ta´ala):

نَبِّئْ عِبَادِي أَنِّي أَنَا الْغَفُورُ الرَّحِيمُ وَأَنَّ عَذَابِي هُوَ الْعَذَابُ الْأَلِيمُ

“Wajulishe waja Wangu kwamba: Hakika Mimi ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu na kwamba adhabu Yangu ndiyo adhabu iumizayo.”[1]

وَإِنَّ رَبَّكَ لَشَدِيدُ الْعِقَابِ

“Hakika Mola wako ni mkali wa kuadhibu.”[2]

[1] 15:49-50

[2] 13:06

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 55-56
  • Imechapishwa: 08/02/2023