Tofauti kati ya matarajio na matumaini:

Kutaraji kunakuwa kumeambatana na kujitolea juhudi na mategemezi mazuri. Kuhusu matumaini yanakuwa yameambatana na uzembe. Amesema (Ta´ala):

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ

“Hao wanaowaomba [wao wenyewe] wanatafuta kwa Mola wao njia [na] kumkurubia kadri wanavyoweza, na wanataraji Rahmah Yake na wanakhofu Adhabu Yake.”[1]

Kutafuta njia ya kumfikia ni kutafuta njia ya kumkurubia kwa mapenzi, ´ibaadah ya kumtii na aina nyenginezo za ´ibaadah[2].

Kwa hiyo ni lazima kwa mtu kuhakikisha matarajio yake. Asiyafungamanishe isipokuwa na Allaah. Asiyafungamanishe na nguvu, kazi yake wala asiyafungamanishe na kiumbe. Miongoni mwa yaliyopokelewa kutoka kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) ni kwamba amesema:

“Mtu asimtarajii mwingine isipokuwa Mola wake na wala asiogope isipokuwa dhambi yake.”[3]

[1] 17:57

[2] Tazama ”Madaarij-us-Saalikiyn” (02/36).

[3] Tazama ”Hilyat-ul-Awliyaa´” (01/76).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 55
  • Imechapishwa: 08/02/2023