33. Dalili kuthibitisha kuwa kutaraji ni ´ibaadah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya matarajio ni Kauli Yake (Ta´ala):

فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا

“Hivyo anayetaraji kukutana na Mola wake na atende matendo mema na wala asishirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote.”[1]

MAELEZO

Matarajio maana yake ni kukipupia kitu sambamba na hilo moyo ukamili kukifikia. Matarajio kwa maana hii, ikiwa mtu atakusudia kwa matarajio hayo kujikurubisha kwa Mola wake, basi itakuwa ni miongoni mwa vitu vinavyofanya kupata radhi Zake. Mambo yakishakuwa hivo kwamba ni katika mambo yanayofanya kupata radhi na mapenzi Yake, basi itakuwa ni ´ibaadah. Kwa sababu ´ibaadah ni jina lililokusanya kila anachokipenda Allaah na kukiridhia. Kwa hivyo ni lazima kumtakasia ´ibaadah ya matarajio Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

Atakayemtekelezea ´ibaadah asiyekuwa Allaah amefanya shirki. Kwa mfano ataraji kuwa maiti atamwingiza Peponi na akamtaraji asimwingize Motoni.

Kuhusu matarajio ya kawaida mtu akataraji kwa mwingine amsaidie, amkopeshe na amsaidie kutengeneza gari ni jambo linalofaa. Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا

“Hivyo anayetaraji kukutana na Mola wake na atende matendo mema na wala asishirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote.”

Kinacholengwa ni pale aliposema:

يَرْجُو

“… anayetaraji… “

[1] 18:110

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 54
  • Imechapishwa: 08/02/2023