hapo utapata faida mbili:

  1. Faida ya kwanza: Ni kufurahi kwa fadhila za Allaah na kwa Rahmah Zake. Kama alivyosema Allaah (Ta´ala):

قُلْ بِفَضْلِ اللَّـهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ

”Sema: “Kwa Fadhila za Allaah na kwa Rahmah Yake, basi kwa hayo wafurahi.” Hayo ni kheri kuliko wanayoyakusanya!” (Yuunus 10 : 58)
  1. Faida ya pili: Umefaidika pia kuwa na khofu kubwa.

MAELEZO

Ukiijua elimu ya uhakika huu basi utafaidika faida mbili:

Faida ya kwanza: Unafurahi kwa fadhila za Allaah kwa vile amekutunuku kuitambua haki kutokamana na batili. Hakika hii ni neema kubwa walionyimwa nayo watu wengi. Amesema (Ta´ala):

قُلْ بِفَضْلِ اللَّـهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ

”Sema: “Kwa Fadhila za Allaah na kwa Rahmah Yake, basi kwa hayo wafurahi.” Hayo ni kheri kuliko wanayoyakusanya!” (10:58)

Fadhila za Allaah ni Uislamu na rehema Yake ni Qur-aan. Kwa hiyo wafurahi furaha ya kuishukuru na kuitambua neema. Kufurahia neema za Allaah ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa kuwa ni kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa neema ya Tawhiyd na kutambua shirki. Ukiongozwa kwa neema hii basi umekusanyikiwa na kheri zote. Kufurahi kwa ajili ya neema ni jambo limewekwa katika Shari´ah. Furaha iliyosemwa vibaya ni kufurahi kwa ajili ya dunia. Amesema (Ta´ala):

وَفَرِحُوا بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا مَتَاعٌ

“Wamefurahia kwa uhai wa dunia. Uhai wa dunia ukilinganisha na Aakhirah si chochote isipokuwa ni starehe ya muda tu.” (13:26)

Kufurahi kwa ajili ya dunia ni jambo lenye kusemwa vibaya.

Kuhusu kufurahi kwa ajili ya dini na elimu yenye manufaa ni mambo yaliyowekwa katika Shari´ah kwa kuwa Allaah ameyaamrisha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 51
  • Imechapishwa: 26/11/2016