35. Hitimisho ya “Sharh Kashf-ish-Shubuhaat”

Kwa kumalizia ni lazima Tawhiyd itendewe kazi kwa moyo, mdomo na matendo. Iwapo atamwabudu Allaah pekee kwa moyo wake – kwa madai yake – lakini akashirikisha kwa mdomo wake au kwa matendo yake hakutomfaa chochote. Au akamwabudu Allaah pekee kwa moyo na mdomo wake lakini akashirikisha kwa matendo yake kama mfano wa kumsujudia mwengine asiyekuwa Allaah na akamchinjia mwengine asiyekuwa Allaah, au akamwabudu Allaah pekee kwa matendo na kwa moyo wake lakini akamshirikisha Allaah kwa maneno ambapo akaomba pamoja na Allaah au akawataka msaada wengine wasiokuwa Allaah, yote haya hukumu yake ni moja. Ni lazima Tawhiyd iwe kwa moyo, mdomo na matendo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 130
  • Imechapishwa: 27/10/2021