34. Uwajibu wa kuitendea kazi Tawhiyd kwa moyo, mdomo na matendo

Kisha mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) akamalizia kwa maneno makubwa ya kwamba Tawhiyd ni lazima iwe kwa moyo, kwa mdomo na kwa matendo. Kwa msemo mwingine ni lazima kwa mtu aamini moyoni ya kwamba Allaah pekee ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa, ayatamke na ayatendee kazi hayo. Endapo mtu atamshirikisha Allaah na akasema kuwa yeye anaamini kuwa Tawhiyd ni haki na kwamba Allaah ndiye anastahiki kuabudiwa, lakini hata hivyo hataki kwenda kinyume na watu wake na kwamba atafanya vile wanavofanya wao katika kuabudu makaburi pamoja nao na kuchinja kwa ajili ya mwengine asiyekuwa Allaah japokuwa anajua kuwa matendo hayo ni batili. Lakini anachotaka ni kuwapaka mafuta watu wake na hataki kwenda kinyume nao, kama walivyofanya makafiri wa Quraysh na wengineo ambao walijua haki. Amesema (Ta´ala) juu yao:

قَدْ نَعْلَمُ إِنَّهُ لَيَحْزُنُكَ الَّذِي يَقُولُونَ ۖ فَإِنَّهُمْ لَا يُكَذِّبُونَكَ وَلَـٰكِنَّ الظَّالِمِينَ بِآيَاتِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ

“Hakika tunajua kwamba yanakuhuzunisha yale wanayoyasema. Hakika wao hawakukadhibishi wewe lakini madhalimu wanakanusha alama za Allaah.”[1]

Amesema kuhusu makafiri wa wana wa israaiyl:

وَجَحَدُوا بِهَا وَاسْتَيْقَنَتْهَا أَنفُسُهُمْ ظُلْمًا وَعُلُوًّا

“Wakazipinga kwa dhuluma na majivuno na hali kuwa nafsi zao zimeziyakinisha. “[2]

Amesema kuhusiana na Fir´awn:

قَالَ لَقَدْ عَلِمْتَ مَا أَنزَلَ هَـٰؤُلَاءِ إِلَّا رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ بَصَائِرَ

“Akasema: “Hakika umekwishajua kwamba hakuna Aliyeteremsha haya isipokuwa Mola wa mbingu na ardhi kuwa ni dalili za kuonekana dhahiri.”[3]

Lakini alipinga na akafanya kiburi.

Kadhalika iwapo mtu ataamini kwa moyo wake ya kwamba Allaah ni wa haki na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni wa haki, lakini akasema kwa mdomo wake kwamba hakuna makatazo ya kuwaomba watu na kuwataka msaada, yote haya kwa ajili ya kuwapaka mafuta watu wake. Vinginevyo anaamini kinyume na hivyo. Mtu huyu atakuwa  ameshirikisha kwa sababu amejuzisha kwa kule kunyamaza kwake na amefanya yale aliyoharamisha Allaah ilihali anajua kuwa ni shirki na akayafanyia kazi. Akisema kuwa yeye hayaamini lakini anayafanya kwa sababu ya kuwapaka mafuta ambapo akamsujudia asiyekuwa Allaah na akaomba mwengine asiyekuwa Allaah amemshirikisha Allaah. Au akasema Tawhiyd kwa mdomo wake lakini akaipinga kwa moyo wake, kama wanavofanya wanafiki, anakufuru. Amesema (Ta´ala):

يَقُولُونَ بِأَفْوَاهِهِم مَّا لَيْسَ فِي قُلُوبِهِمْ

”Wanasema kwa midomo yao yale yasiyokuwemo katika nyoyo zao.”[4]

لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ

“Hivyo msitoe udhuru, kwani mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.”[5]

Haijalishi kitu hata kama watasema kuwa nyoyo zao ni nzuri na zimesalimika. Midhali amefanya shirki na mambo yenye kupelekea katika ukafiri.

[1] 06:33

[2] 27:14

[3] 17:102

[4] 03:167

[5] 09:66

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 129-130
  • Imechapishwa: 27/10/2021