35. Amezembea kulipa siku anazodaiwa mpaka kumeingia Ramadhaan nyingine

Swali: Nilizembea kulipa baadhi ya masiku niliyokuwa nikidaiwa katika Ramadhaan iliyotangulia mpaka kukaingia Ramadhaan nyingine. Ni kipi kinachonilazimu?

Jibu: Kimsingi Allaah (Ta´ala) anatwambia:

فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu au yuko safarini, hivyo basi akamilishe idadi katika siku nyinginezo.”[1]

Allaah amemruhusu msafiri kutofunga. Badala yake amemfanya alipe masiku mengine. Allaah hakuweka wakati maalum wa kuyalipa, lakini ni lazima yalipwe ikichelewa sana mpaka Sha´baan. Ikiwa masiku anayodaiwa yanalingana na idadi sawa na siku zilizobaki za Sha´baan, basi  analazimika kuharakisha kuyalipa katika Sha´baan. Asipofanya hivo, basi anapata dhambi. Aidha atatakiwa kuyalipa masiku anayodaiwa ya Ramadhaan iliotangulia baada ya Ramadhaan inayofuata pamoja na kumlisha masikini kwa kila siku moja anayodaiwa. Vilevile anatakiwa kutubu kwa Allaah kwa ucheleweshaji usiokuwa na udhuru.

[1] 2:184

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 33
  • Imechapishwa: 08/04/2022