34. Mfanyakazi anayesafiri hadi 400 km kufupisha swalah

Swali 34: Mimi ni mfanyakazi katika kituo cha treni ninakagua tikiti na wakati mwingine nasafiri na treni hadi umbali wa 200 km na wakati mwingine hadi 400 km. Je, inafaa kwangu kufupisha zile swalah za Rak´ah nne[1]?

Jibu: Kujengea yale uliyoyataja inafaa kwako kufupisha kutokana na umbali uliotajwa. Ni masafa yanayozingatiwa ya kufupisha. Imetuthibitikia, baada ya kutafiti, ya kwamba umbali unaozingatiwa kufupisha ni takriban 80 km na zaidi.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (11/267-268).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 50
  • Imechapishwa: 08/04/2022