35. Kufupisha na kukusanya kwa ambaye siku zote yeye ni kusafiri

Swali 35: Vipi kuhusu kufaa kufupisha na kukusanya swalah kwa yule ambaye mazowea yake ni kusafiri kutoka Saudi Arabia na kwenda nchi za nje au kutoka katika baadhi ya miji ya Saudi Arabia na kwenda katika baadhi yake ambayo inafaa kwa msafiri kufupisha na kukusanya kama vile madereva wa magari na wengineo walio na hukumu kama wao katika wafanyabiashara na wengineo[1]?

Jibu: Hawa wana hukumu moja kama wasafiri. Imewekwa katika Shari´ah kwao kufupisha swalah. Inafaa kwao kukusanya kama wasafiri wengine kwa mtazamo wa kikosi kikubwa cha wanazuoni kutokana na kuenea kwa dalili za ki-Shari´ah juu ya hilo. Hatujui dalili inayopingana na hilo.

Kuhusu maneno ya baadhi ya wanazuoni kwamba si mwenye kunuia kukaa mji maalum na hivyo haifai kwake kuchukua ruhusa za safari ni maoni ambayo ni dhaifu. Hatujui wajihi wake kutoka katika Shari´ah. Hayo yamezinduliwa na Abu Muhammad bin Qudaamah (Rahimahu Allaah) katika “al-Mughniy”.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (11/269).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 51-52
  • Imechapishwa: 08/04/2022