06. Aina ya tatu ya watu kuipokea Ramadhaan

3 – Wako wengine ambao Allaah (´Azza wa Jall) amewaneemesha kwa maafikisho, akawachunga kwa uangalizi Wake na akawazunguka (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa uangalizi Wake ambapo wakaziandaa nafsi zao kwa ajili ya Ramadhaan. Utamuona mbele yake ana fikira nyingi na akilini mwake kunazunguka aina mbalimbali za mambo ya kheri. Hivyo utamuona anapanga wakati kwa ajili ya Ramadhaan, wakati kwa ajili ya kumtaja Allaah, wakati kwa ajili ya kusimama usiku, wakati kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji, wakati kwa ajili ya kutoa na wakati kwa ajili ya vikao vya elimu. Wakati unakuwa mfinyu kwake.

Watu wengine wanaona kuwa mwezi unawabana kwa sababu ya kuwa na miradi mingi, kazi nyingi na mambo mengi kwa ajili ya kumtii Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Lakini hata hivyo mwezi unambana na hapati muda kutokana na wingi wa yale mambo ya kheri alionayo.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Wa jaa´ Shahru Ramadhwaan, uk. 09
  • Imechapishwa: 08/04/2022