4 – Kuna aina nyingine ya watu matangamano yao na Ramadhaan ni kama wanavotangamana na miezi mingine yote. Ramadhaan inampitikia kama inavyompitikia miezi mingine yote. Kiasi cha kwamba, mpaka ule mwezi ambao imetajwa ndani ya Qur-aan kuwa ni kheri kuliko miezi elfu moja, inawapitikia watu wengi kama inavyowapitikia miezi mingine yote. Hii ni hasara mbaya, kughilibika kwa wazi na upotofu usiyomstahikia kumtokea muislamu. Kwa ajili hii muislamu anatakiwa kufanya vizuri kuupokea mwezi huu na kumpokea vizuri mgeni huu. Aiandae nafsi yake ili awe miongoni mwa watu wa mwezi huu kwa ukweli na kwa haki.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Wa jaa´ Shahru Ramadhwaan, uk. 09-10
  • Imechapishwa: 08/04/2022