Swali 34: Ni lini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipewa ruhusa ya kuhajiri?

Jibu: Wakati washirikina walipoona kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameshakuwa na wanusuraji na wasaidizi na kwamba Maswahabah zake wameshakuwa na mji salama wa kuhamia na ndugu wa kweli wa kuwasaidia na kuwanusuru, ndipo wakakusanyika ili kumfanyia vitimbi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Walikuwa na chaguo tatu: kumfunga jela, kumuua au kumfukuza. Hatimaye wakakubaliana juu ya kumuua, khabari aliyoipata kutoka mbinguni. Wakati vijana wao walikuwa wamesimama nje ya nyumba yake wakiwa wamezichomoa panga zao na kungoja wamuue, akaenda juu ya paa lake, akiwasomea mwanzo wa Yaa Siyn na akiwarushia mchanga juu ya vichwa vyao. Hawakuhisi kitu mpaka pale ambapo tahamaki wakaona kuwa mtu ambaye walikuwa wanamchunga alikuwa ni ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye alikuwa amelala kwenye kitanda cha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawakujua ameshika (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) njia gani[1].

[1] Ahmad (1/303).

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 103-104
  • Imechapishwa: 01/10/2023