33. Dini ya Allaah ambayo kawatuma kwayo Mitume wote

na umeilewa dini ya Allaah ambayo amewatuma kwa ajili yake Mitume, kuanzia wa mwanzo wao mpaka wa mwisho wao, ambayo ndio dini ya kipekee ambayo Allaah anaikubali kutoka kwa mtu

MAELEZO

Dini ya Mitume ni Uislamu. Uislamu ni kujisalimisha kwa Allaah kwa Tawhiyd, kunyenyekea Kwake kwa kumtii na kujitenga mbali na shirki na watu wake. Hii ndio dini ya Mitume na huu ndio Uislamu.

Kuhusu kujinasibisha na Uislamu kwa nje pasi na ndani, kujinasibisha kwa kujiita peke yake pasi na kushikamana na zile hukumu zake, kujinasibisha nao na wakati huo huo mtu akawa anafanya shirki na mizimu yanayoutengua, kujinasibisha nao na wakati huo huo mtu akawa anajahili uhakika wake au kujinasibisha nao pasi na mtu kuwapenda wapenzi wa Allaah na kuwachukia maadui wa Allaah, sio Uislamu waliokuja nao Mitume. Ni Uislamu tu wa kiistilahi usionufaisha kitu mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Isitoshe hii sio dini ya Mitume.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 49
  • Imechapishwa: 21/11/2016