82. Dalili ya kwamba matendo mema yanamfikia maiti

Kumeshatangulia ya kwamba Allaah (Ta´ala) anasema:

وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ

“Na wale waliokuja baada yao wanasema: “Mola wetu! Tusamehe sisi na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa imani na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo ya chuki kwa wale walioamini. Mola wetu! Hakika Wewe ni Mwenye huruma, Mwenye kurehemu.” (59:10)”

فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ

“Basi tambua ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na omba msamaha kwa dhambi zako na [omba msamaha] kwa ajili ya waumini wa kiume na waumini wa kike!” 47:19

الَّذِينَ يَحْمِلُونَ الْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيُؤْمِنُونَ بِهِ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَيْءٍ رَّحْمَةً وَعِلْمًا فَاغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا وَاتَّبَعُوا سَبِيلَكَ وَقِهِمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ

“Wale wanaobeba ‘Arshi na walioizunguka wanasabihi kwa himidi za Mola wao na wanamwamini na wanawaombea msamaha wale walioamini [kwa madhambi yao]: “Mola wetu, Rahmah na elimu [Yako] imekieneza kila kitu! Hivyo basi, wasamehe wale waliotubu na wakafuata njia Yako, na wakinge na adhabu ya Moto.” 40:07

Yasingeliwanufaisha basi Allaah asingeliyataja kwa njia ya kuvutia.

Kuhusu Hadiyth, Imaam Ahmad na an-Nasaa´iy wamepokea kupitia kwa al-Hasan bin Sa´d bin al-´Ubaadah ya kwamba mama yake alifariki. Akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Mama yangu amefariki. Nimtolee swadaqah?” Akasema: “Ndio.” Akasema: “Ni swaqadah ipi bora?” Akasema: “Kunywesheleza maji.” al-Hasan amesema: “Ni mnyweshelezo wa familia ya Sa´d uliyoko al-Madiynah.”

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa kuna mwanaume alimwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Baba yangu amekufa na hakuacha anausia. Itamnufaisha nikimtolea?” Akasema: “Ndio.”

Ameipokea Muslim, Imaam Ahmad, an-Nasaa´iy na Ibn Maajah.

´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza ya kwamba kuna mwanaume alimwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Mama yangu amekufa. Lau angeliweza kuzungumza angelitoa swadaqah. Anapata ujira lau nitamtolea swadaqah?” Akasema: “Ndio.”

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na Imaam Ahmad.

Ibn-ul-Mundhir amepokea kwa mlolongo wa wapokezi wake kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kwamba aliacha mtumwa huru kwa ajili ya kaka yake ´Abdur-Rahmaan baada ya kufa.

ad-Daaraqutwniy amesimulia kuwa al-Hasan na al-Husayn walikuwa wakiwaacha watumwa huru kwa ajili ya baba yao ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) baada ya kufa kwake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 178-179
  • Imechapishwa: 21/11/2016