83. Tafsiri ya Aayah “mwanadamu hatopata [malipo] isipokuwa yale aliyoyafanyia bidii”

Baadhi ya walioenda kinyume katika Shaafi´iyyah na Maalikiyyah wametumia hoja kwa maneno ya Allaah:

وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ

“Na mwanadamu hatopata [malipo] isipokuwa yale aliyoyafanyia bidii.” 53:39

ya kwamba maiti hanufaiki kwa matendo ya wengine. Isitoshe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi w sallam) amesema:

“Pindi mwanaadamu anapofariki basi matendo yake yote hukatika isipokuwa vitu vitatu; swadaqah yenye kuendelea, elimu yenye kunufaisha au mtoto mwema mwenye kumuombea du´aa.”

Wanasema kuwa manufaa ya ´ibaadah hayamnufaishi mwingine isipokuwa yule mwenye nayo tu.

Wanarudiwa ya kwamba imethibiti katika Sunnah na maafikiano juu ya kwamba maiti anaswaliwa, anaombewa du´aa na kuombewa msamaha. Matendo haya si yake, ni ya wengine. Kadhalika wao wenyewe wanakubali kuwa maiti ananufaika kwa kule wengine kumtolea swadaqah na kumwachia watumwa huru baada ya kufa kwake. Kile watachosema juu ya suala hilo lililo na maafikiano ndio jibu juu ya suala lililo na mivutano. Wanachuoni wameijibu hoja hiyo juu ya Aayah hiyo na ipo katika vitabu vikubwa. Lakini baada ya ukaguzi mtu ataona kuwa Allaah hakusema kuwa mwanaadamu hanufaiki kwa matendo ya wengine. Alichosema ni kuwa:

وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ

“Na mwanadamu hatopata [malipo] isipokuwa yale aliyoyafanyia bidii.” 53:39

Mwanaadamu hamiliki isipokuwa kile alichofanya mwenyewe. Hastahiki zaidi ya hicho. Lakini yale wengine wanamfanyia ni yake pia. Ni kama vile mtu anayemiliki pesa zake mwenyewe lakini anaweza vilevile kunufaika na pesa za wengine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 182
  • Imechapishwa: 25/11/2016